RAYA & BALATA AQDI!!!

BRIDE                       ::RAYA RAMADHANI
GROOM                    ::BALATA ORKASH
EVENT                      ::ISLAMIC AQDI
VENUE                      ::TABATA
BRIDAL MAKEP    ::MAZNAT BRIDAL CARE
COLOR                     :: BLUE & SILVER
NI AQDI YA RAYA NA TABARI WAPENDANAO LEO WAMEKUWA KITU KIMOJA , SHANGWE ZILISIKIKA HUKO MITAA YA TABATA BIMA, NDOA ILIFUNGWA HAPO HAPO NYUMBANI, RAYA SIMPLE KAPENDAZAJE NA HINA YAKE....!!! FOLLOW ME INSTAGRAM "MASHUGHULIBLOG", KUZIONA SHUGHULI KAMA HIZI WAKATI WA TUKIO

 HINA...!!!

RAYA AKIINGIA
DECOR.....///
RAYA AKISAINI CHETI CHA NDOA NA MUME WAKE AKIMPA MKONO
KISHA WAKAPENYWESHANA MAZIWAWAKWE WAKIPELEKA SANDUKU
BURUDANI
CHAKULA
MAHABATI
NYUSO
WIFIE & FRIENDS
SOMO, RAYA & MDOGO WAKE RAY
MAMA YAKE RAYA
MAMA MZAZI WA TABARI
TIFFA & FRIEND
ALHANISA SLEYUM NA MZAZI WA TABARI
MAMA MZAZI WA RAYA NA SHANGAZI
WIFIE RAYA
RAYA & FRIENDS
SOMO NA MWARI WAKE
MAMA NA MWANA
MAARUSI NA MAMA NA MAMA MKUBWA
RED CARPET
 TIFFA KASEMBO

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

11 comments:

 1. mashaalwah Mola awape faraja
  MAZIWA yana maana kubwa sana hapo. Mie shoga angu aliolewa ilikuwa mpya ikaletwa cheni bwana akafungwa mguuni na mguuni kwa mke kaa pingu nadhani mnanipata mjuao harusi zetu za kiislam . Wakaoshwa miguu basi mama yake Siri akachukua maji akenda nayo jikoni akatia kwanye Glas akatia na maji ya bomba . Mwisho akpewa mume anywe . Dada nilifatilia kaa naangalia Film nikauliza ninini ? Jibu unamweka mwanaume miguun ,ile ya kumshusha nyota mtu .Hapo ndo nachokaga ntawapa nyingine

  ReplyDelete
  Replies
  1. shoga hiyo sio mpya labda ilikua mara yako ya kwanza kuhudhuria ndoa za kiislam hiyo ni ya kuvalishwa cheni mguuni ni sehemu ya harusi bwana harusi anaoshwa na maji ya zamzam halafu anafungwa cheni yeye na msimamizi wake bwana tumbili kafungwa halafu ndio anakalishwa kula solo ukikuta zile shughuli zimezingatiwa kwenye ndoa hiyo lazima iwepo ila mambo ya siku hizi na uzungu umeingilia utakuta mambo kama haya yanarukwarukwa mradi ndoa tu ipite
   na hiyo mambo ya kuangalizia nyota yapo yanafanyika kabla ya ndoa Shekhe anaangalia majina ya maharusi kama mwanamke jina lako limezidi nyota kali unapewa jina la ndoa utasikia jina lake la ndoa bi fulani na hata wakati ndoa inafungwa basi jina la ndoa hutumika wanashusha ile nyota ili zilingane hakuna nguvu za giza kama unavyofikiria hiyo ipo kuanzia ndoa ya mtume na bi Khadija

   Delete
  2. unapojibu angalia unajibu nini maziwe ni suna na kisha wanatakiwa wasali rakaa 2 kumuomba mmungu awape masikilizano na kuwaepushia mitihani ya ndoa hakuna cha cheni wala maji ya zamzazm hayo ni mambo ya kidinia sheria ya dini yetu hayo hakuna tunawatakia harus njema

   Delete
  3. Hiyo ya kufungwa cheni na kuoshwa miguu si uislamu bali ni ndoa ya ushirikina. Kwa kunyeshwana maziwa ni Sunna kwa maharusi kufanya hiyo. Ndoa ya kiislam ni baada ya hutba ya kungishwa ndoa, bwana harusi anaingia ndani kumpa mkono mkewe , kumshika kichwa na kumsomea dua kisha anamnywisha maziwa, Hizo nyengine zote ni mbwembwe ambazo hazina faida yoyote katika ndoa. Upumbavu unamnywisha mtu maji machafu akipata kipindupindu na kufa ndio takua umeshusha nyota mpaka kaburini..

   Delete
 2. Mashallah Raya ulipendeza.Allah akulindie ndoa yako na akupe kizazi chema in shaa Allah.
  Umekuwa mkubwa nakukumbuka toka sinza, mama yako aliolewa na marehemu mzee Nyasenga ,Allah arehemu.
  Nimemuona mama Rose na mama Mwafatima, wapi mama Boa?wakina mama wa Sinza wakali.Mungu awape afya njema wazee wetu na wote walotangulia mbele ya haki Allah awarehemu in shaa Allah

  ReplyDelete
 3. Si kweli kwamba ni utaratibu wa dini kuangalia nyota. Huo ni USHIRIKINA TU NA UJAHILIYA wa kutojua UISLAMU!! Bi Khadija na Mtume wetu mtukufu hawakufanya hayo. Hizo ni mila tu za wasiojua DINI. Fuatilieni na muulize. Tena hao wanaoangalia nyota au majina wanaongoza ndoa zao kuvunjika. Fuatilia na utapata majibu kama ninavyosema. Uislamu ni mwepesi hakuna hayo

  ReplyDelete
 4. mashallah mungu awazidishie maisha mema ya ndoa yenu na sisi tuliobaki mungu atujalie tufunge ndoa tuwe kama nyie. amina

  ReplyDelete
 5. Mashallah harusi nzuri Mungu awajalie kila la nimempenda wajina bi latifa kapendeza mno toka kitchen party Mashallah

  ReplyDelete
 6. Msichanganye habari hayo maziwa na sijui, cheni miguuni na kutazama nyota, ni tabia na mila za watu, it is nothing to do with islam. ni mambo zaidi ya kipwani. Msiuharibu uislam. ila bahati mbaya watu wa pwani wengi ni waislam ndio maana inaonekana inafanywa kiislam. LAKINI la ni mila za watu na sio uislam jamani. futa usemi wako.

  ReplyDelete
 7. Jamani inabidi mjuae mnayoyasema si kusema tu kupotosha watu uislam hauna ndoa ya kufungwa cheni mguuni wala kuangalia jina la mtu wala habari za nyota, katika Qur'an tukufu mambo yakuangalia nyota yamelaaniwa, sasa iweje ndoa ya muislam au waislam wanaojua dini waangalie nyota? mnaitia uharamu ndoa bila kujua then mnategemea ikawe ndoa njema.

  ReplyDelete
 8. Maziwa ndiyo katika misingi ya uislam bi Aisha r.a alipoolewa na kipenzi chetu Muhammad s.a.w alinyweshwa na maziwa kisha bi Aisha naye akamnywesha Mtume lkn kuangalia jina haliendani na nyota sijua cheni hivyo havipo katika mafundisho ya Mtume jamani tusomeni dunia yetu na akhera yetu ili tusidanganywe na wale wasiojua dini na kuingia katika shirki.

  ReplyDelete