Ndoa ya Bomani ya Big Halima Juma na bwana Hija Saleh

 Baada ya kufunga ndoa miaka mitano iliyopita sasa nimeamua kuhitimisha ya bomani bwana na bibi Hija Salehh & Halima Juma bonyeza kitufe kwa picha zaidi


Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

12 comments:

 1. sijaelewa ndoa ya mwanzo ilikua ipi sasa ya pili ya bomani kwani dini gani hawa au sijui kusoms vzr naomba majibu pls

  ReplyDelete
  Replies
  1. makaratasi hayyo mdau,ukiishi ughaibuni utayaelewa zaidi

   Delete
 2. Ukiona hivyo ujue ni ndoa ya kiislam ambayo nafikiri kwa huku kwa wenzetu haitambuliki au kukubalika katika mambo ya makaratasi, mfano mmoja wenu akiwa mwanafunzi mmoja labda ana ukaazi wa kuishi sasa mplk yule mwingine akubalike kisheria ya nchi lazima wapitie ndoa ya bomani,hasa kama mmefunga ndoa ya kiislamu

  ReplyDelete
  Replies
  1. wee bibi acha uongo kudanganya watu ndoa zote zinatambulika duniani iwe ya kristo iwe islamu hao maharusi watakua na sababu zao wanazijua wenyewe vyeti vyote vya ndoa Tanzania ni vya aina moja kinachozidi ni mahala mlipofungia ndoa kama ya kanisani inatiwa muhuri wa kanisa kama ya kiislamu inatiwa muhuri wa bakwata haya wewe mwenzetu unacho hata hicho cheti? au unachonga tu kutaka kukandia ndoa za wenzenu? weka heshima dada ndoa ni ndoa hata ile ya kutoroshana ni ndoa fungua macho uone heshima kitu cha bure nina mengi ya kukwambia ngoja niishie hapa

   Delete
  2. nimekupenda mdau hapa uliemjibu wa juu, una uelewa mkubwa.. elimishisha elimisha washamba wengine wasiouelewa uislam siwapendi wanajuaga kusema ya hovyo na akili zao za kijinga shabash

   Delete
  3. marahabaaa mdau uliemjibu huyo juha nachukiaga kuna wana dharau na ndoa za kiislamu tena msomi na kwenye familia yake ukute ana wanandugu waislamu lakini anajifanya haelewi muwe mnachukua muda kujielimisha maswala ya dini zote msikae gizani ulimwengu mwingine huu, yaani kwa akili yao ndoa ni kanisani tu na matarumbeta nikuulize mdau wazazi wako hata cheti cha katibu tarafa hawana lakini ni wanandoa msonyooo

   Delete
 3. duh lemba la bi harusi nimelipenda balaaa.. asante mashughuli kwa kutuwekea vitu vizuri mweh

  ReplyDelete
 4. Mimi naona mdau hapo wa pili hujamuelewa ana maana gani ndoa zote halali ila cheti lazima kiwe cha kiserikali kama huku uarabuni hata ukifunga ndoa bongo na uneolewa na raia wa huku inabidi mpate kibali tena cha serikali na kuapishwa na kadhi sio kwamba wanakidharau cheti ulichokuja nacho kila nchi ina sheria hiyo fungua macho tembea uone mimi mwenyewe nimebadilishiwa cheti cha ndoa kwa hiyo cha bongo sikitumii tena hukumwelewa naona umemrushia mvua ya maneno

  ReplyDelete
 5. mdau wa u turn blogDecember 25, 2012 at 9:43 PM

  makaratasi@work hakuna cha ndoa ya bomani wala nini hapo,wa ughaibuni tumeshaelewa mapema,wabongo ndio shida,yote maisha,chezea makatasi wewe

  ReplyDelete
 6. hahaha haluuu cna la kusema mabo paper tu

  ReplyDelete
 7. jamani kuweni waelewa ndoa ya kiislamu haina cheti cha sericali tofauti na ndoa ya kikristo. ndio maana mdau kasema uwezi vuka boda bila cheti cha ndoa cha serikali. du ndugu zangu acheni ubishi someni mjue.

  ReplyDelete
 8. nadhani wadau wote inabidi mpewe elimu juu ya sheria .
  kwanza lazima utambue kila nchi inasheria zake
  pili lazima ujue kuwa vyeti vyote ni halali bali kuna nchi hasa ulaya marekani hata asia na ukirudi afrika lazma uwe na vyeti vinavoeleweka mfano hapo nchi jirani ya kongo tunayopakana nayo uitaka kuishi au kwenda kusalimia lazma uwe na vyeti vitatu vya ndo moja ni cha dini yako uwe mkristo, muislam au mhindu, pili cheti cha ndoa za kimila so lazima urudi kwenu ukafunge hiyo ndo na tatu lazima bomani
  so tatu lazima ujue na uelewe sheria hizo zote zina kusaidia wewe mwenyewe incase mumeokafa au umepata ajali ya kufa wewe familia yako itasave mana mali na watoto watalindwa kwa haki zote
  sasa huyo mdau wa pili alierusha maneno naomba aende rita waone kuwa wanatoa vyeti vyote co vya kuzaliwa na kufa bali hata cha ubachelor ili ukienda nchi nyingine huko nje usifukuzwe na pia vya ndoa vipo kwa jili ya wenye ndoa ili ukienda uwe unatambulika
  mwisho kabisa tusome ndugu wanainchi tujue sheria na haki zetu hapa nchini na nje ya nchi la sivyo mtaumia msidhani hizo ndoa na kutoroshana ni dili si dili mdau fuata sheria kama hujaolewa fuata yafuatayo: lazima uwe na vyeti hivi:
  1 chakuzaliwa
  2 vya shule kuanzia chekechea mpaka ulipoishia kama o level au a level
  3 vya vyuo ulikosoma
  4 cha dini yako
  5 passport halali
  6 nenda rita kachukue cha ubachelor hapo utakuwa salama
  kwa wenye ndoa hapo mnakuwa navyo vyote including cha ndoa zote za kidini na bomani ikiwezekana tafuta cha kimila pia mwisho nenda rita pata cha ndoa na wewe utakuwa umefanikiwa

  mwisho kabisa tuache matusi na kejeli wote ni sawa nadhani dada mashughuli atafurahi zaidi tukitenda yaliyo mema na kuendelea kusoma na kuelimishana basi tuwe na heshima na ustarabu siku njema wadau wenzangu asante kwakusoma hayo machache hapo juu

  ReplyDelete