MARYLINDA & DAVID WEDDING! - NAIJA

 Make-up!


MARYLINDA & DAVID FRIENDS PARTY-PARTY2MARYLINDA & DAVID TRADIONAL WEDDING IN CALABAR


Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

9 comments:

 1. Shukran bi helen kwa kutuonyesha hata arusi za nija. Nakupenda sana helen. Kwa kutuonesha arusi hizi nina hakika una maana nyingi tu ikiwa ni pamoja na kutuonesha shughuli sehemu tofauti tofauti lakini pia kutufunza, na kutonesha ni jinsi gani wenzetu wa naija kwanza, wanavojipamba, kwa maana ya hassa make up; jamani hebu tuone na tubadilike kwani wenzetu jamani, upakaji wa makeups zao ni almost 'natural' zinapendeza mno, kwani poda kwa kiasi, eye shadow kwa kiasi, lipstick kwa kiasi, na si kujikandika kama vile tunausongo nazo yaani, hata ule uzuri wa mtu alojaaliwa na Mungu unapotea, hapendezi.!!
  Pili, jamani, kingine ambacho kwa kweli nil lazima, lazima tujifunze na sisi jamani, vizuri mbona vyaigwaaa!!! Wenzetu wanaheshimu mno tamadulni zao na wanazitukuza mno, hili kwa kweli lazima tuwapongeze sana, mila zao hawaziachi.

  Kwa kweli nakupongeza helen kwak utuonesha kwa wingi picha hizi ni kweli kabisa tumeona na tutazidi kukumbushana hadi nasi tubadilike!! kwani tunavoona zaidi ndivo tutajifunza zaidi, hata ikibidi nasi kuandaa shughuli zetu za kimila na kufanya iwe ni part ya sherehe za arusi yaani kwa kuvaa nasi mila za tamaduni zetu. jamani, tubadilike!! kwani - VIZURI VYAIGWAAA!!!!!!!

  ReplyDelete
 2. Da Helen unajituma sana na kwa kweli unafanya vizuri sana kutuonnyesha mambo ya nje big up my dada good day.

  ReplyDelete
 3. jamani make up zao ni kiboko.na nawasifu sana kwa kufata tamaduni zao.sio sisi tamaduni zetu tunazitupa.siku hizi kila harusi kwaito.mdundiko na vanga hakuna tena

  ReplyDelete
 4. ee la ajabu ni hilo kwaito ni ngoma ya wenzetu, wakati na sie tunaZetu nzuri tu, imagine mdundiko ulivo jamani au mkwaunguma na kadhalika, mbona tuna nyingi tu kwanini hatuchezi za kwetu, sasa imekua ngoma ya watu ndo fashion, kila arusi ndo hiyo hiyo, mmmm tunapenda mno kuiga jamani, tuthamini vyakwetu, mbona vitapendeza tu tukivifanyia ukarabati kidogo kwani taarab si hiyo ipo lakini imefanyiwa ukarabati na bado ni taraab ile ile, na inapendeza tu hata kama ni modern tarab lakini bado ni tarab; so na nyingine tunaweza kufanya hivyo hivyo zikanoga tu, WE CAN MAKE IT - LET US CHANGE!!!!

  ReplyDelete
 5. @ dada hapo juu.hujaenda sherehe za uswazi ???? ngoma ya baikoko sasa hivi ndiyo inatamba.huu ni mdumange kutoka kwa wasambaa lakini watu wengi wanaalika kwenye sherehe zao na inafurahisha na kusherehesha.

  ReplyDelete
 6. thanxs anty helen. nashawishika kuwashawishi wazazi wangu kwenye harusi yangu kuwe na mila hata kama ni kwa upande wa wanawake tu.

  ReplyDelete
 7. dada umesema hiyo kwaito ninavyoichukia, kila ukienda harusini watu wanaona sifa hao wasouth wenyewe wameiga kwa wamarekani weusi basi ni muendelezo tu wa kuiga lkn kitu akipata mtanzania inakuwa mbaya zaidi wakati mwingine watu wakianza natamani nitoke kwenye shughuli.

  ReplyDelete
 8. wenzetu wana jitahidi sana lakini sisi bado hatujawafikia na wanadumisha sana mila yao

  ReplyDelete