WANA TANDAMTI KARIAKOO WAFUTURU PAMOJA NA WATOTO YATIMA!

 Mtaa wa Tandamti uko Kariakoo, hawa mie nawaita wana wa Tandamti, mara nyingi hufanya Maulidi na sasa wameongeza ili la kufuturisha kipindi cha Ramadhani, ni jambo nzuri kuona vijana wanaungana na kuwajaali watoto yatima!!!
 
 
 
 

 Vijana wa mtaa wa Tandamti wakiserve chakula
 Mshindo akifuturu pamoja nao!!

Watoto wakipata zawadi kwa ajili ya sikukuu

Baada ya zawadi zao mwalimu pamoja na watoto waliomba dua!! 


Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

10 comments:

 1. Hongera zenu wana watandamti tumefurai sana

  ReplyDelete
 2. mashaala mungu awazidishie...........

  ReplyDelete
 3. Mashallah inshallah m/mungu atawalipa kwa mema yenu mnayoyatenda.

  ReplyDelete
 4. Ni jambo zuri sana kuwafikiria wale ambao wanastaki msaada hasa katika siku kama hizi za Kheri. Mwenyezi Mungu atawalipa zaid ya mlichotumia. Mama jr

  ReplyDelete
 5. mashalaah mungu awabaariq..!awaongezee zaidi ya hicho walichokua nacho,,nawafuturishe zaidi ya hao watoto inshlh kher!

  ReplyDelete
 6. Mashaallah shughuli imependeza vijana wa Tandamti wamejitahidi, Allah awape ujira wao Inshaallah!

  ReplyDelete
 7. Mashallah kila mwenye kutenda jema ktk mwezi huu mtukufu jazaa yake iko kwa mungu. Asante dada hellen pia kwa kutuwekea mambo yanayokhusu kwenye mfungo Mungu akubariki angalau na sisi wa mbali tunaona matukio muhimu kama hayo

  ReplyDelete
 8. Inapendeza inavutia sana.
  M'mungu awazidishie na kuwatia imani wote waliofanya shughul hii.

  K

  ReplyDelete
 9. Si vyema kwa Waislaam kuwakusanya watoto yatima na kuwalea kwenye vituo vya yatima au kuwaita na kuwalisha chakula kwa pamoja.

  Uislaam unataka yatima umelee kama mwanano na inapaswa kila Muislaam badala ya kuchangia kuwalisha chakula, kuchangia kuwalea kwenye vituo, ni vyema angechukuwa yatima amlee kama mwanae.

  Wasilaam tujilinde sana tunaweza kuona tunafanya jema kumbe si jema bali ni janga. Hili la kuwachukuwa watoto yatima na kuwaturisha ni janga si jema.

  Yatime umlee asijijuwe kama yeye ni yatima, kama unavyowalea wanao nyumbani.

  Hivi kuwakusanya na kuwaonesha kuwa wao ni wakusaidiwa tu, unawafundisha nini? au unajitafutia umaarufu kwa jina la yatima?

  ReplyDelete
 10. mmmh nimepita tu

  ReplyDelete