MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU YALIYOANDALIWA NA AISHA SURURU FOUNDATION (ASF)

Venue: Diamond Jubilee hall Masheikh ambao ni majaji, kila kitu kilikuwa computerized.
Watoto wa kike washindani
Picha za vijana mbalimbali katika kusoma Qur'an tukufu na kuulizwa maswali ya papo hapo

Huyu kijana ni kipofu, lakini uwezo aliojaliwa na Mweyezi ni wa ajabu ameweza kuhifadhi Qur'an juzuu  10 kichwani na aliulizwa maswali ya papo hapo na majaji, ametokea Pemba yeye hakuwa katika mashindano alialikwa  na Taasisi ya ASF

Mgeni rasmi Dk Hussein akiuliza swali
Mama Aisha, mke wa Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akimuuliza swali kijana toka pemba
Picha za watoto wa kike walioshindana
Kijana huyo alipewa shillingi 500,000/= kama zawadi yake
Picha za upande wa kike
Joha Lemki katibu wa Taasisi ya Aisha Sururu Foundation akisoma risali kwa mgeni rasmi na waalikwa

Mgeni rasmi upande wa kiume alikuwa Dr. Mwinyi
Picha mbalimbali za Dr. Hussein Mwinyi akisoma risala katika hafla hiyo
Certificates of Appreciation 
Watu mbalimbali walishiriki katika kufaniksha hafla hii ya mashindano ya Quran, walipewa vyeti vya shukurani na taasisi ya ASF
Matokeo
Jaji kiongozi akitangaza matokeo
Zawadi ndogo ilikuwa ni 150,000/= na mshindi wa kwanza alipata millioni 2.5 na pikipiki.
Mshindi wa kwanza alihifadhi Qur'an juzuu 30, alipewa millioni 2.5 na pikipiki, kama tujuavyo bodaboda ni biashara kwa hiyo ni njia moja ama nyingine ya kusaidia kuelekea kwenye Maisha Bora kwa kila mtanzania.
Mgeni rasmi na yeye alipata zawadi toka kwa Taasisi ya ASF
Washindi wakiwa na zawadi zao, ikiwa ni pamoja na vitabu vya dini, vilivyotolewa na Taasisi ya Rehema

Wanawake
Mama Aisha Bilali ndio alitoa zawadi akisandikizwa na Aisha Sururu Mwenyekiti wa ASF

Katoto haka alishinda shillingi 1,250,000/=

Taasisi ya Rehema Foundation wakitoa zawadi za vitabu na vitambaa vya nguo ya sikuku kwa upande wa kike
Mshindi wa kwanza upande wa kike akipokea pesa taslim 2,500,000/=
Hapa akikabidhiwa bodaboda yake!!
Washindi katika picha ya pamoja
Mama Asha na Bi Eshe Sururu katika picha na washindi wa kike

Wakati wa mapumziko kulikuwa na wageni toka Iran wakiomba dua kwa kughani!!


Sheikh mkuu wa msikiti wa Idrisa, sheikh Ally akitoamawaidha


Skauti wa kiislamu wakimuonyesha mgeni rasmi walivyo wakakamavu

Cerificate of Appreciation 
upande wanawake
Wanawake walijumuika pamoja na ASF katika kufanikisha hili, walipata vyeti cya shukurani
Nyuso
Aisha Sururu Mwenyekiti wa ASF, akiwa pamoja Aisha Bilali mke wa makama wa raisi
ukumbi mkubwa wa Diamond, ulijaa takribani watu 5000, hawa ndio wazazi na wapenzi wa Quruan Futari

ASF walifuturisha watoto yatima na watu mbalimbali jioni hapo hapo Diamond Jubilee
 
 
 
 
 
 
 
 
                         
                         
 
 
 
 
 
 
 


Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

10 comments:

 1. Mashaallaah Hellen,M.mungu azidi kukujaalia na moyo huo huo wa kuijali na kuithamini dini ya kiislam,tunakushukuru saana kwa kutuletea mambo ya dini kama haya katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu alhamdullillah.

  ReplyDelete
 2. Shukran sana Hellen kwa picha nzuri kwa wakati kama huu,Ubarikiwe sana; AMEEN. Waisilamu wakike ni vyema tukawa na staha kama hizi wakati wote si wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan tu, kwani tazameni wenyewe mlivyopendeza mashallah!!! mashallah!! na wala haihitaji tochi, ni dhahir tena natural!!. Mwezi huu Mtukufu ni kipindi cha mtihani kwa Waislamu, tuukabili mtihani huu na tuwanie kushinda/kupasi na si kushindwa; kwani tukinuia tutaweza. Mwanamke akijisitiri kwa kweli inapendeza na anapendeza sana na kwa waislamu ndio wajib. Tujitahid basi kuendeleza vivazi hivi si kwa mwezi Mtukufu tu wa Ramadhan bali kwa miezi mingine yote. Mungu atujaalie sote turudi kwenye iman na tutekeleze vyema mambo mengi pamoja na stara - ameen.

  KILA LA HERI HELLEN ZIDI KUTULETEA PICHA KAMA HIZI, ZINATIA HAMASA SANA KWA WAKATI HUU NA HATA BAADAE UKIJAALIWA.

  ReplyDelete
 3. mashallah!mungu awafanyie wepesi na awazidishieni nguvu muweze kufanya na ramadhani zijazo in shaa allah!

  ReplyDelete
 4. MASHAALAH YOTE YAMESHA SEMWA...AMEEN

  ReplyDelete
 5. Mashallah shughuli imependeza na inatia moyo.

  Hellen blogu yako ni HAKUNAGA, Mungu akujalie kila la kheri, na amjaalie aliyeandaa hiyo shughuli pia!

  ReplyDelete
 6. mungu atujalie tufanye shughuli nzuri kama izi inshaallah huu ni mfano mzuri wa kuiga. mama ulie andaa hii shughuli allah akulipe inshaallah

  ReplyDelete
 7. Mashaallah.
  dada nimependa sana umeheshimu mwezi mtukufu na pia kuonesha jinsi gani ni wa muhimu huu mwezi ktk maisha ya waislam. hakika Allah atakulipa malipo yalo mema leo na kesho akhera. jazakallah kheir

  ReplyDelete
 8. Mungu akujaze kheri dada hellen

  ReplyDelete
 9. Hellen kweli wewe huachi kitu mungu akupe wepesi kwenye mambo kama haya picha zimependeza wanawake wamevaa kwa kujisitiri - mungu amjaalie aliyefanya shughuli hii na ampe uwezo wa kuendeleza dini kwa vijana wetu wawe na maadili mema.

  ReplyDelete
 10. MashaAllah, bi Aisha Sururu anafanya kweli, Mwenyeezi Mungu amzidishie.


  Shamim Khan vipi? na Bakwata na siasa zao hata kwenye maendeleo ya Waislaam? naona Sheikh Lion na Shamim Khan wakiona hivi wanasema MashaAllah.

  ReplyDelete