WEDDING RECEPTION DINNER OF SAJJAD & KIWAKO

Venue:: Urban Rose Restaurant
Seleman Mathew akituongoza kwa niaba ya familia, kulikuwa hakuna MC
Dr. Tamba akifungua shughuli kwa dua

Chakula


Pete & Cake
Malaika wakikabidhi pete kwa maarusi 
 Pete za Sajjad & Kiwako
ZawadiNyuso


Sherry & Sango
  Sherry & Isabella
 Hajary, Hellen & Sophia
 Mama wa bi harusi

 Asha & wifiye!!!
 Shangazi Bishara wa ukweee'e
 Bishara & Beuty
 Mama na Mwana

 Mariam & Halima
 Muhaza, Hajjary & Hawa!!


 inapendezaje, Bishara na wakwe zake Mr & Mrs Tamba


 Mr. & Mrs. Tamba
  
 Mama na wana!!! Mzee, Bishara's husband

 Mama na Mwana,mtoto kwa mama hakui..!!

 happy couples!!!

Red Carpet
Halima

  Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

20 comments:

 1. manshaalaah maharusi mmependeza sana mungu awabariki ndoa yenu iwe ya amani na furaha

  ReplyDelete
 2. simple na imependeza kikubwa wakadumu katika ndoa yao inshallah,latifa nassor umenenepa mashaallah

  ReplyDelete
 3. Mashallah kwangu mimi hii ndio wedding ya mwaka, kuanzia ukumbi simple na msafi hauna yale makapeti machafu mnaita sijui red carpet; hakuna makorokoro sijui mapambo. Hakuna mashauzi ya mijikeki huku mkisubiri madeni (maana keki za show off ni za malaki) au watu kuadhiriana wewe sijui hujatoa mchango; hakuna kupakana mijasho sijui rusha roho, everything is on point, simple islamic wedding sio vya kuigaiga visivyo kichwa wala miguu kutakufuta ugomvi na watu.

  Nimeipenda hii, na pia nimeupenda huo ukumbi panapo majaaliwa nataka kufanya shughuli yangu hapo ya watu kama 50 au 100 basi. Hongera sana maharusi kwa kufanya mambo yenu simple bila kuweka RIYA!!

  ReplyDelete
 4. haruc simple haina makorokoro wala tafrani sa roho,, mola awape maisha marefu ya ndoa hadi mfanane sura...

  ReplyDelete
  Replies
  1. arusi ni nzuri sana.Bibi harusi ni mrembo sana lakini hajapata wa kumpamba vizuri angekuwa mzuri zaidi ya hapo kama angepata mpambaji mzuri japo ni mrembo sana

   Delete
 5. Wewe anonymous wa tatu unaesema hii ndio harusi ya mwaka, kwanza hii recepetion dinner na sio ndoa ambamp ndio ungesema arusi ya kiislam, arusi ya kiisalam haina mambo kama haya!! na kama unasifia sifia tu kama wengine usinze kukandia shughuli za wengine wakati kila mtu na uwezo wake, wewe fanya hiyo kwako usimchangishe mtu wala nini wanaochangiana! mnafiki mkubwa wewe!!! kama ulidaiwa kwa snn hujachanga ndio ukome kama ulichangiwana wewe lazima uchange, HARUSI NI HIYARI YA WATU KILA MTU ANAPENDA YEYE MWENYEWE HAFANYAJE.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Eee dada wewe ndio wale wale nini wakutembea na kadi kudai watu michango? Maana naona umerukwa na fahamu kwa kusema "Kwangu mimi hii ndio harusi ya mwaka" Rejea tena sentensi yangu, uifahamu vizuri, sikusema kwa kila mtu, nimesema kwangu mimi, wala sikulazimishi upende kile ninachopenda mimi.

   Baada ya kukufafanulia kuwa kuwa huo ndio utashi wangu, nataka kukwambia hivi sio mimi peke yangu tu watu wengi wamechoshwa na mabakuli ya michango; mtu pato lako kwa mwezi lets say laki 5, kwa mwaka 500,000 x 12 ni 6,000000; unatakaje kufanya harusi ya gharama ya milioni 20? Au hata milioni 10? Kisa kutegemea michango? Kwanini usifanye yaliyo ndani ya uwezo wako?

   Kuhusu mimi eti sichangii, nachangia sana mpaka nimechoka maana hakuna shughuli nyingine za maendeleo kama kuchangia elimu watoto waende secondary tumekalia kuchangia maharusi na mashughuli kila siku. Mimi niliolewa zamani, harusi yangu kwa taarifa yako kila aliyeweza kutia mguu wake alikuja, ilikuwa ni open wedding, baada ya ndoa watu wakala karamu (walimat-lharusi) mie na mume wangu tukaenda zetu nyumbani kwetu; hakuna cha reception wala nini. Hatukumchangisha mtu wala mume wangu hakutozwa mahari ya ajabu, (elfu 30 tu)na miaka hiyo nimeolewa ndio kwanza nimemaliza Masters yangu. Sasa hivi mimi na mume wangu tuna watoto wakubwa 4 na ndoa yetu ina miaka 18 sasa. Na hata nikitaka kuoza mtoto wangu panapo majaaliwa nitafanya family & close friends tu ndani ya uwezo wa familia yangu basi!

   Mwisho harusi ya kiislamu ina kitu kinaitwa Walimat-lharusi, yaani chakula kinachoandaliwa na upande wa mume kulisha watu kutangaza hiyo harusi baada ya ndoa kufungwa na mfano wa hiyo walimat-lharusi ndio waweza kuwa hiyo dinner hapo juu.

   Delete
  2. Nimekupendajee dada hapo,kwa kweli ukweli ndio huo,kila ulichoongea ni point na mfano wa kuingwa,too much ujinga siku hizi.

   Delete
  3. Yaani dada ningekua karibu ningekutunza. Viatu vinaisha soli kwa kudai michago. Ahsante Mungu kwa kuniondosha huko mda mdogo niliofanya kazi niliiona kasheshe maana mtu utasema kakupa umshikie...

   Delete
 6. Nimependa sana hii harusi, ni mara yangu ya kwanza kucomment ila nimevutiwa sana na harusi

  ReplyDelete
 7. Wewe anonymous hapo juu wa saa 11.22, soma msg ya mwenzio vizuri nathani hujamuelewa! kasifia tu kwa nia njema!

  ReplyDelete
 8. Hey there, I think your website might be having browser compatibility issues.
  When I look at your blog site in Firefox, it
  looks fine but when opening in Internet Explorer, it has
  some overlapping. I just wanted to give you a quick heads up!
  Other then that, fantastic blog!
  My web-site ; hcg canada reviews

  ReplyDelete
 9. i like this its kind of family and close friends only. may Allah bless them. Luvs it

  ReplyDelete
 10. very simple. Wow nimeipendaje. Hivi ndo nataka harusi yangu iwe Inshaallah

  ReplyDelete
 11. Mashughuli umetisha mpaka kwa wahindi upoo! hongera kwa maharusi. Tunawaombea ndoa yenye utulivu.

  Sherehe naona ilikuwa na utulivu pia

  ReplyDelete
 12. Very simple & nice party,you look mmmwaaaaaa....

  ReplyDelete
 13. Nimeipenda hii harusi yani iwe mfano wa kuigwa simple aina makolokolo mengi hadi raha!

  ReplyDelete
 14. mashughuli umeitendea haki hii shughuli kwani umependeza sana hakuna kitu kizuri mtu kujua uvae nini kwenye shughuli gani, sio mtu anavaa kimini kwenye wedding reception. hii shughuli ukweli ni kwamba watu wote wamependeza sana.

  ReplyDelete
 15. If you are going for finest contents like me, simply pay a quick visit this web site everyday for the reason that it offers quality
  contents, thanks

  Feel free to surf to my website: similar website

  ReplyDelete
 16. Naona kama Bi Harusi Mchina!!! kipenda roho. kila la kheir katika ndoa yenu. Wachina hawana tabu, tabu ipo kwetu, Kijana utulie na mkeo.

  ReplyDelete