AQDI YA MTUMWA NA ABDULKADIR

Venue:: Cutchi Hall
Bride:: Mtumwa
Groom: Abdulkadir
Entertainment:: Rusha Roho
Decoration:: Princess Latifa (Fatuma Chizenga)
Colour:: Light Blue & Gold
Make-up:: 
MC::
Caterer::Pincess Latifa
Mtumwa akiingia ukumbini
  
aliingia huku akirusha roho


  
Mume naye akiingia na mpambe wake
Mtumwa akianguka kuthibitsha kauli yake!!!
Mlisema hayawi mbona yamekuwa, vyeti hivi hapa!!! kitu kimoja sasa
Mke wangu kipenzi!!!
Pete
  Picha za Malavidavi...!!!
Decor
Chakula
Nilishe nikulishe ndio ishare ya upendo, mtumwa unadeka eeh!!
Cheza
Mtumwa akirusha roho na mashostito
Kidole juu
Tunza
  

 

  Mawifi wakienda kutunza

Hapa naona niongee kidogo, jamani kwa nini hatujui dress code ya shughuli, kwa kawaida ukiambia ndoa tena ya kiislamu lazima ujue jinsi ya kuvaa, sasa huyu msichana alikuja na hiyo nguo akashindwa kunyanyuka mpaka kwenda kutunza!! kwa nini unajipa taabu mwenyewe watu wote wanakutazama wewe!! au ukija hivyo ndio utaonekana unajua fashion?? ushamba tu, anayejua kuvaa ufahamu dress code, mimi watu kama hawa wananiboa sana!!! kuharibu tu shughuli za watu!!!

   Mwaka akitunza mihela hiyoooo!!!
   Chezea Mwaka wewe
   unatambaje Mtumwa!!! wamekuona eeh! na wewe una watu wako eeh!!
Wadau samahanini sana ngoja niongee na hapa kidogo tena, sasa hii ndio nini? kuna shughuli zakufanya hivi kama vile kwenye singo lakini sio siku ya Aqdi jamani, mnatuonyesha picha gani hata kama bi harusi ni shostito wenu, hapa kuna watu wengi mama zake, wakwe zake, wifi zake kama  ni mfanyakazi na wafanyakzi wenzio, mimi niliona waalikwa wakiguna!! hata bibi Mtumwa hakupenda!! tuwe wastaarabu jamani, ustaarabu hauuzwi ni bure tu!!! kama kwenye singo binuka mpaka!!!, wapiga picha hatukupata picha nzuri kwa sababu na fujo zisizokuwa na msingi!!!

Nyuso

Red Carpet

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

10 comments:

 1. Hongereni maarusi ALLAH ajaalie ndoa ya amani usikizano na upendo tele INSHA ALLAH.

  Anty Hellen kwani hii harusi haikua na MC akawakataza hao wajinga wa dunia?. bada Aqdi iwe na barka wanamletea wenzao nuksi tuu shenzi kabisa. Alafu anty kwanini huongelei na swala la nywele na makeup?.

  ReplyDelete
 2. Nadhani wenye harusi wenyewe ndo wameprovoke hiyo mizuka,rusha roho ya nini kwy aqdi!

  ReplyDelete
 3. Anty Hellen ungezungumzia pia habari ya nywele na make up kama ni harusi ya kiislam basi baadhi ya kina dada wangefunika vichwa vyao.

  ReplyDelete
 4. Mdau wa mwisho, nimeona bora nikujibu, 1. kwanza kabisa mimi ni mkristo na sidhani kama italeta maana nikiaaza kuwaambia mabiharusi wafunike vichwa vyao will make sense, 2. ninaheshimu uhuru wa mtu na ninaamini kila mtu anafahamu dini yake inamtaka afanye nini. 3. mimi niko kikazi zaidi na siyo kwamba shughuli zote hizi ninawafahamu hapana sasa nikiaanza kuwananga watu kuhusu make-up nadhani hata picha ninazowaletea hamtazipata ili nyie wadau mnaweza toa somo kwa njia yoyote ile,Na hii ya Mtumwa ndoa ilifungwa msikitini na bwana arusi akaja mpa mkewe mkono ukumbini.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mimi ni muislamu na ninakuunga mkono 110%; hivi mtu tangu uko mdogo unalelewa kwenu hata kama hukusoma madrasa lakini maadili ya dini ya kiislamu yako wazi, leo hii mtu mzima ndio uje kufundishwa kuvaa?

   Sasa bora hapo ni kwenye harusi na kwenye hall, utakuta mtu mwingine anakwenda kwenye hitma au msima kajipura minywele kama kinyamkela inahuu?

   Da Hellen sisi wengine huwa tunajua character ya mtu kutokana na marafiki zake, kwa mfano mimi kamwe marafiki zangu hawawezi kufanya viroja vyovyote kwenye shughuli yangu, wazungu wanasema birds of same feathers fly together, huwezi kumkuta kinega anaruka na kundi la mabata au kunguru!

   Delete
 5. Mawazo yangu mie naona hakuna ubaya wowote, arusi ilifungwa msikitini, badala ya bwana arusi kwenda nyumbani kumpa mkono bi arusi, alikwenda holini, inategemea kila mmoja na uwezo wake na mipango yake, wameamua kimalizia holini, si si vibaya, kwani hapakua na wanaume, shughuli ilikua ya wanawake tu kwa hiyo sioni ubaya wowote wa bi arusi kuwa alivyokuwa, inawezekana pia baada ya kula mumewe hakukaa maana hatuoni katika picha kuwa alikuepo au kama alikuwepo basi hapakua na wanaume wengi, naona hakua mbaya kwa kweli, tuelewe arusi ni mipango ya mtu na mipango ya asha inaweza isifanene ya ya fatuma, mana kila mmoja anafanya, kwanza kwa uwezo alokua nao pia kwa apendavyo, mwengine atakua na shughuli ya siku 7, ataifanyia nyumbani mpaka maholini, mwengine atafanya simple siku moja na akaamua isiwe nyumbani iwe holini ... haya maona yangu.

  ReplyDelete
 6. Mashughli kila mara huwa nataka nikuulize wewe dini gani?maana huwa naona maongezi yako,na kazi yako huwa umeekeza sana kwa Waislam,,sasa kitu ambacho huwa kinanichanganya ni jina lako (Hellen)..Kweli leo nimeupata ukweli,ndo nimezidi kukuadmire kabisaaa!,,maana ungekuwa muislama ningekutilia ulakini wa ubaguzi wa Dini!
  Mimi nimekupendaje dada,unaonekana ni mama mwenye maarifa ya hali ya juu,Insha'Allah nikija'aliwa kuja nikutafute unisaidie kitu flani.
  Pia hiyo uliyosema kutoingilia maswala ya watu katika shughli zao,ni kweli,,kama umeenda pale kama mpiga picha,ni kweli hiyo kazi lazima ina limit yake.Na kama ungeenda pale kama MC,,ndio ungekuwa na uwezo wa kuongelea kuhusu hao waliocheza na wala sio kuzungumza habari ya makeup..maana hiyo inakuwa haikuhusu,,
  Watu hawaelewi jamani,,kuhusu hizo makeup au sijui nywele,ni mtu kuambiwa na ndugu yako alokushiba au rafiki yako wa karibu mno,au kama kina mama mnajumuika pamoja mnaanza kuelimishana kuhusu kuzidisha makeup si vizuri maana mtu unaonekana kama kinyago hivi,hata kinyago kina nafuu,maana hakimove lakini wewe unaonekana kama jini maana unaongea na kucheka etc.
  Na hata hivi ulivyoandika katika blog ni kwa ajiri yetu sisi wasomaji wa blog,wala sio kwa hao walengwa wenyewe,,hata hivyo kila mara watu wanalalamika humu kuhusu makeup,,inaishia hapa hapa kwa wasomaji,,otherwise mtu ana ndugu yake akisoma humu kisha akaenda kumwambia ndugu yake au rafiki yake ya kuwa wadau wa MASHUGHULI wanalalamika makeup kwa hiyo punguza,na hiyo tu inaweza kusaidia
  Kila la Kheri Hellen!
  Mpenzi wa Mashughli Blog
  Ahlam..London

  ReplyDelete
 7. Kwanza Hongera zao maharusi, Mungu awape kheri kwenye ndoa yao.
  Biharusi nguo yake ni nzuri, Rangi pia imeendana na hata kuta za hall. Tatizo ya sisi waislamu, tuna assume kila mtu atajua cha kuvaa kwenye shughuli zetu, wakati mashosti zetu wengi sio waislamu. Ilimbidi bi harusi aseme kwenye kadi ya mualiko mavazi yanayotakikana kuvaliwa. Na hao mashosti, ilibidi atoke Shangazi moja kuwaambia waache.

  ReplyDelete
 8. Bi harusi mwenyewe kichwa kipo wazi unategemea mashost watavaaje.
  i agree birds of same feathers fly together

  ReplyDelete
 9. Kuamrishana mema kupo na kukatazana mabaya kupo, tusichoke pale Wadau wanapofanya ndivyo sivyo basi tukemee. Pia katika Aqdi ya Kiislam jamani Vichwa na kwa kweli hata Bibie mwenye shughuli naye alijisahau. Pengine ni kutokana na furaha ya siku yake. HONGERA MAHARUSI NA MUNGU AWAFUNGULIE KIZAZI CHEMA CHENYE KUFUATA MAADILI YA DINI.

  ReplyDelete