SINGO YA MWANAHAMISI KARIAKOO LIVINGSTONE


 Hamadi na kibao kata akiwapagaisha watu, umeshaisikia nyimbo mpya ya kumuenzi Kanumba ya kibao kata?? nitawaletea soom!!!
wenye sare zao za kijani walikuwepo kibao mwishowe wakagombana wenyewe kwa wenyewe 
 watu walichezaje!!!

 wewe huyo Zuhura
 kila mtu akionyesha ujuzi wake!!! mama Tanisa mwali wa Tanti Boy nakuaminia!!


 umeona eeh!! huyo alibinua kama nusa saa hivi!!! chezea wa kariakooo!!

 ngoma bila kucheza nitaichezajeee mie, kweli bila ya kupombeka haiwezekani


Fatuma Kibao msasambuaji maarufu balaa tupu, ukitaka kusasambuliwa naye tuone mashughuli, sisi tunakuletea wale ambao hujui pa kuwatoa!! hajali mjomba wala shangazi ndio kazi yake!!! 

 Designer Bahiya yeye anasema ni mkali wa don't take my number yeyoooo!!!
 Mwishowe kwaito
bi harusi matarajiwa Mwanahamisi, katolewa nje baada ya kusingwa!!
Somo wa Mwanahamisi Tanti a.k.a Boy Super Star, akiwa na Faiza Mafish

Tatu Lumelezi, mimi nalia na COMING SOON!!, Mariam Best & Friend
Tanis Mwaibula, Tanti Boy & Faiza Mafish

Rehema & friend

Bibie Lumelezi & Friend
Mwali wa Bijoha
Shumu na nduguye

hawa walikuwa wanakata mauno chini kwa chiniHadija Ndombolo, akisimama ndio utajua maana ya ndombolo ya solo!!! enzi za tazara wapiiii!!!
bi mdanga chezea yeye livingstone hiyo


Hafsa & Friend
mama ya Athuman & shumu

Faiza & friend
Mafish family!! wapi bi Saada Brazak hapana ona yeye, salam zake nasubiri dira
Isabela & friend
Shumu na Dalila a.k.a Jembe


Jembe supu bado??
Hawena

Mshindo & Adam, nyie mnawalinda dada zenu eeh!!!

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

14 comments:

 1. Mie napenda sana kuangalia blog hii, kwanza inatuonyesha matokeo ya arusi na kupata mwangaza wa mambo mengi yanayohusiana na arusi, kitchen party na kadhalika. Pia hata kwa upande wa picha pia ni nzuri kwa kweli, nakusudia quality. Kwa kua ni mpenzi wa blog hii, naona nina haki ya kutoa ushauri/nasaha au mawazo.

  Napenda kutoa maoni yangu kama mtumzima. Nasema kweli kabisa ndani ya nafsi, picha kama hizi hazifai kutolewa kwa kuonekana na watu wote. Zamani kibao kata kilikua mithili ya unyago. Ngoma hii huchezwa na wanawake watupu na huwa hairushi au kuonekana na watu wengine kama wanaume na watoto wadogo, ni wale tu waliohudhuria sherehe kwa wakati husika. Unyago ndio kabisaaa, unakua ni kwa wanawake pia ngoma haipigwi picha zikaonekana na kila mtu. Sasa mara hii kutoa picha kama hizo hapo juu kwa kweli haipendezi. Picha si nzuri na blog inaangaliwa na watoto, wanaume, wakubwa kwa wadogo. Naona hii itavunja hadhi ya blog na pia haitoleta maana nzuri ya ngoma yenyewe na maudhui ya blog. Pendekezo langu kwa blog kama mpenzi wa blog hii, kwa nia safi kabisa ningependekeza picha aina hii zisionyeshwe kwa kila mtu kuona.

  Samahani sana endapo nitakua nimeandika kitu ambacho hakitafurahisha watu/mwenye blog...

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mawazo yenu ni mazuri na kweli ni bora achague picha za kuweka na hao mnaowaona hapo si wanaume full ndo maana wako hapo.

   Delete
 2. kwa kweli namuunga mkono huyo mtowa maoni hapo juu ndio sisi tulio mbali na kwetu tunapenda kuangalia hii blog kwani tunapata kuwaona ndugu,marafiki,wapenzi wetu lkn hizi picha zingine its to much.i think u should select what to show on ur blog.

  ReplyDelete
 3. ni kweli kabisa blog inataka kupoteza uzuri kwa kuweka picha za namna hiyo

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ni kweli kabisa, nawaunga mkono wadau wenzangu waliotangulia kuchangia hii mada, tulianza vizuri kuona picha nyingi za shuhuli tofauti na zilikuwa nzuri sana lakini tunakoelekea sasa sijui. VERY BAD. Tujirekebishe jamani tusiharibu hadhi ya blog yetu.

   Delete
 4. Mimi naamini Bi mashughuli atakuwa ameelewa,kwani hakuna binadam aliyekamilika.shughuli ni watu na watu wenyewe ndo sisi..Nakupongeza sana Bi Mashughli,kwani wewe unastahiri SIFA,nimependa sana ulivyoamua kupost hizi comments za hao waliotanguli hapo juu!Inaonyesha kweli unatujali saaaaana kuliko nilivyotegemea,,najivunia na naamini sasa hii blog ni ya kwetu sisi wote!AHSANTE SANA,NA UBARIKIWE MNO!

  Mimi mwenyewe Binafsi nimepunguza kuangalia blogs za uchi uchi yaani nina maana ya picha zinazomfanya mtu ashuke Imani yake katika kumcha Mwenyezi Mungu(Nafikiri wadau mnanielewa ni blog gani).Ila nimechagua baadhi ya Blog ikiwemo my favourite blog(MASHUGHULI),ambayo nikiikosa nakosa raha kabisa..

  Nakupongeza mdau wa kwanza kwa kujiamini na kuweza kuthubutu kutuma hiyo comment kabla hujajuwa Bi Mashughli ni mtu wa aina gani,,na baada ya kutuma wewe na wengine wakapata nguvu ya kutuma walipoona kumbe Bi Mashughli ni MTU WA WATU
  JAZZAKALLAHU KHAIRAN

  AHLAM,,,LONDON

  ReplyDelete
  Replies
  1. Ahlam, hakuna blogu Bongo ambayo wanawake wamevaa nguo inavyotakiwa kama unazungumzia kutokana na imani na mafundisho ya kiislam, maana wote wako uchi, kwani unaelewa ni maeneo yapi ya mwanamke ambayo hayatakiwi kuonwa na watu wengine isipokuwa maharimu wao au wakiwa na wanawake wenzao. Sasa hapo kwenye hii Post si kuna wanawake wako vichwa wazi, mabega wazi, matiti yanaonekana, miguu, wengine shape za body zao zinaonekana hata kama wamevaa skin tight au stockings. Kwa hiyo hilo la kusema eti nimechagua baadhi ya blogu kwa sababu zinamfanya mtu ashuke imani sikuelewi? Kwa mfano humu kunakupandishaje imani yako? Nafikiru uwe unakwenda Alhidaaya, Quran explorer, deenislam na blogu nyingine ambazo zina maandishi tu hazina picha. Vile vile usiangalie TV hata BBC news, Aljazeera au channel yoyote ile isipokuwa channel za kidini hapo ndipo utasalimika, otherwise ndio itakuwa design ile ya waislamu wanakunywa pombe kisha anakuja juu akiletewa nyama ya nguruwe ale, akidai kadhalilishwa nguruwe kwake haramu; wakati uharamu wa nguruwe ni sawa sawa na uharamu wa pombe, sawa sawa na uharamu wa kusengenya, kusema uwongo, lakini haufikii uharamu wa kuzini ambao umepitiliza. Lakini utakuta mtu anaogopa kula nguruwe ni haramu huku anakunywa pombe na kuzini.

   Cha msingi hapa ni hizo picha za xxx ambazo zimewakwaza wengi, nafikiri ni ushauri mzuri uliotolewa kuhusu hizo picha ili kulinda maadili na kusudio za hizo ngoma, za kufundishana mambo ya ndani. Lakini tusiingize dini kabisa kwenye haya maana kwa dini ya kiislamu hakuna cha ngoma, muziki, sijui unyago, sijui kitchen party, hayo tunayafanya kulingana na mila na desturi zetu, basi.

   Delete
 5. ah hao wote waliotangulia kuweka comments nadhani hawajui maaana ya mshughuli blog.mashuguli blog maana yake ni blog ya shughuli zote iwe mbaya au nzuri,shughuli shughuli 2,na wala msiimngize mambo ya dini mkapata dhambi bure pasipo na sababu ya msingi,dini yetu hata kukaa kichwa wazi ni haram,ss kama ww unaona masguhuli wanaweka picha mbaya kiroho saaaafi kbs usiwe unangia,tuachie tunaopenda,nyie wengine mnakasumba mbaya sana,mnata da hellen awe anaweka zile shughui za kifahari 2 za kwenye makumbi,then zilizo local aziache sio? hiyo ss itakuwa inapoteza maana ya mashughuli blog,ss watoto wa k.koo tulio nje ya nchi yetu tunafurahi sana kuona matukio ya mitaa yetu bana,na kuwaona marafiki,jamaa na majirani kupitia mashughuli.acheni hizo bana da hellen endelea kutupia mapicha ya watoto wa mujini,hasa k.koo tupate kuwaona kina bi mdanga,zuhura,tanisa,sara bi dalila,kuwaona kwetu pia ni furaha sana kwa ss tulio mbali na bongo yetu, nakupongeza sana bi mashughuli kwa kazi nzuri sana mm kama fans wa mashughuli nakupa big up sana.
  salma wa chura ...............hapa

  ReplyDelete
 6. Jamani waliochangia hapo juu wanamaana ya maadili ya kitanzania na ya sisi waswahili tunaojua maana ya kibao kata na unyago na sio mambo ya dini ya kiisalam. hizi picha hazifai kuonekana kabisa na watu kama wanaume na haswa watoto ambao bado hawajafikia kuolewa. jamani acheni hizo lazima tufate mila zetu bwana. hata huo utandawazi una mambo yake sio mambo ya unyago na kibao kata hadharani. wewe Hellen hata kama blog yako ni ya mashughuli ndio uweke picha za unyago kwenye blog kweli ni sawa au watu mnapenda kujifanya ndio maendeleo? Maendelo gani hayo acheni bwana. Kuna mambo yakuonyesha kwenye blog na mengine ni furaha yenu wanawake tukikutana tunacheza na kufurahi sasa mnamuonyesha nani kuwa nyie ni mafundi? Hayo ni maoni yangu.Ukipenda fata usipopenda endelea lakini huo ni usungo!!!

  ReplyDelete
 7. Watu wa kariakoo siku hz wamepoteza muelekeo. Sisi tuliozaliwa na kulelewa kariakoo miaka hiyo ya sitini na sabini tulikuwa na miiko sana na tulikuwa tunaongoza kwa kufata miko. vitu kama kibaokata ni ngoma ya siri sana sasa iweje siku hz wapoteze muelekeo mpk walipie picha hizo za unyago ziwekwe kwenye blog. Jamani acheni kufanya mambo yasiofaa bwana. kuna kitchen party, harusi, maulid, birthday na sherehe nyingi tu ambazo hazionyeshi mambo ya ndani, toeni lakini hizi zinatudhalilisha sana. Hata hivyo ngoma hizi siku hizi zimeingiliwa na watu wasiojua maana yake. kama kweli umechezwa unyago huwezi kufanya mambo haya. Poleni sana!!!!

  ReplyDelete
 8. Hapa ndugu zangu, kikubwa zaidi, si mavazi kwani kila mmoja ana hiari yake na mwili wake,kikubwa hapa ni picha za aibu ingawa watu wako kwenye nguo zao lakini 'style' ya michezo iliyoonyshwa haiko kabisa kwenye ngoma jamani, kweli ngoma gani inachezwa kwa michezo aina hiyo, hata huo unyago hauchezwi hivyo. Tunasaidiana kuboresha blog hii na si kuibomoa kwa kutokubali kuwa picha hizo hapo juu si nzuri!!! ingawa hatulazimishani kila mmoja anamtazamo wake, kibaya kushabikia uzuri wa picha wakati tunajua si picha za kawaida kuonekana hadharani na kila atakeona zinampeleka kwenye picha za xx; ILI blog hii iendelee kuheshimika duniani, basi tukubali tu kuwa picha aina hii haizifai kuoneshwa katika blog, wapewe tu wenye shughuli na zichaguliwe zile tu zinazofaa zirushe; manaa kuna blog nyingi jamani duniani aina hii lakini hatujaona picha kama hizi, sasa kwanini na sisi tushikilie ku support kutolewa hadharani kwa picha hizi, inavunja heshma ya blog! hapa hatulaumu shughuli a a a, kinachosemwa hapa baadhi ya picha ambazo si za kawaida ya ngoma tunazozijua kuonekana hadharani, tupambanue vizuri nini tunachoongelea hapa isionekane kuwa tunalaumu ngoma ya watu hapana, tunachosema; hapa kubwa kuonyeshwa aina ya baadhi ya picha zisizofaa kuonekana.!!

  ReplyDelete
 9. make up crisis...goosh!!! my eyes lol!.

  ReplyDelete
 10. Kwanza napenda kumpongeza Sister Helen kwa kutuletea Blog hii yenye kutuletea mambo mbali mbali ya starehe , sherehe,misiba na mambo kadha wa kadha hususan yanayowagusa watoto wa mjini(kama wanavyojiita)au wana Darisalama. Pili nawapongeza wote waliotoa maoni yao hususan mdau wa kwanza kabisa kuhusu uwekwaji wa baadhi ya picha zisizofaa. tukirudi upande mwengine nilikuwa nampinga mdau Salma wa mtaa wa chura aliyekuwa akishabikia. Salma ukumbuke blog hii inatizamwa na watu warika tofauti. vijana na watoto, wake kwa waume hivi Salma leo mama yako mzazi au dada yako, shangazi yako au mkweo atundikwe kwenye blog akiwa amegaragara chini au amebinuka(mikao ya hasara hasara) huku amedandiwa kwa nyuma je wewe utapendezewa na jambo hilo?. tusishabikie tu wakati picha kama hizo zinaweza kuleta athari nyingi tu tukumbuke wengine ni wake za watu au wachumba wa watu picha kama hizo zinaweza leta mvunjiko katika mahusiano kati ya mke na mume , mchumba , mzazi na mtoto au hata pengine ndugu na jamaa. la mwisho ningekuomba Sister Helen usichoke kutuletea habari mbali mbali ila kidogo upunguze makali ya picha .
  mdau Kaka wa Salma San Diego US.

  ReplyDelete