SINGO YA WARI WA SALMA MNTAMBO, YASMIN MBEGU & AZA MNONDWA

 Zawadi ya Aza Mnondwa, aliyoandaliwa na Somo yake Salma Mntambo Bed Room Set, kama alivyotaka yeye ndivyo alivyopata toka kwa shangazie!
Sitting Room Set
 
Microwave & Gas Cooker
Hiyo ndiyo zawadi aliyopewa Jasmine Mbegu, alipewa alichotaka na somoye Salma Mntambo umeona Kabti full viombo vya ukwee'ee, chezea Salma weye!!!
 Table Setting by Shaikha Mgawe wa TPA, ndiye aliyepamba ukumbi, pendeza eeh!!, mpigie simu no.
  Wana wari walikaa hapa!
The only one MC-Jamila Kitmtim
Wari waliingia na chetezo kwa ajili ya kusingwa


 Hii ndio kuokota Mizungu???


Mgeni rasmi alikuwa mama Sitti Mwinyi
Udi ulifuka holi nzima
Salma Mntambo alisaidiwa n Joha Simba, Dalila Jaggar, Mariam Mntambo, jamani siwezi wataja wote ila kama kuchezwa basi Jasmine & Aza wamefaidi 

Tajiri Kubwa Salma Mntambo akiingia kwa Confidence siku zote hakosei hata kidogo

Singo bwana ndio hii, wari hawa hakufunuliwa kabisa, mtawaona kwenye k-party yao, hawakushonewa dira wala nini mambo yalifanywa kama yanavyotakiwa

Mauno ya ukwee'e
umemuona nyakanga Dalilah Jaggari?? pembeni!!!
Wari wakaanzwa kusingwa na masomo, jamani hii ndio maana ya singo, wari hawa wamefaidi mengi sana hata unyago awamechezwa ule wa kizamani....sio wa sasa!!!! hii ndio jeuri ya Salma Mntambo

Salma Mntambo akikabidhi zawadi zao
Da Aza akikabidhiwa zawadi ya mwanae na bi Salma...!!!

Samira mziwanda wa Salma Mntambo akienda mtunza mamaye...!!!Kwa viuno wamejaaliwa mie sina choyo jamani...!!!

Mama Jasmine naye alimtunza Salma akiongozwa na mama NgodaWakaiingia Ma'Diva wa ukweee, pia kumtunza mama

Sharifa Kavu na yeye alimtunza Salma Mntambo, si mnakumbuka somo yake Khadija, sanduku la ukweee mpaka hii hakuna mtu aliyevunja rekodi yake...!!!
Khadija akaenda na mkwe wake pia kumtunza bi Salma

Wacha Picha Ziongee mie tena Basi..!!!Hapa lazima niongee kiduchu, Dalila Jaggari ni MC, Somo na Nyakanga pia sasa yeye ndiye atatuelezea tofauti ya nyakanga na somo....!!!
Si umecheki meza eeeh!! picha zinajieleza zenyewe 


Mariam Mntambo, yeye ndiye supplier wa vinywaji vyote isipokuwa vyenye kilevi , piga simu hii Mntambo shop upate huduma ya kuletewa mpaka hapo ulipo 0713-259050 
Khadija pendeza na mama mkwee!!!
Latifah, mambo bank sio!!! chezea wewe!!! 
TAJIRI KUBWA nani weza wewe??? hakuna bwana!!!!
Happy pendeza shosti mie ona wewe lakini...mmhhh
kama wewe hakuna MADINI MADINI


Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

8 comments:

 1. hiyo sofa set na cofee table ya mwari gani? naomba utujuze maana umetuambia kuwa bedroom set ni ya Aza, jiko la gas,macrowave na kabati la vyombo la jasmin. pia usikose kutuletea picha za kitchen party dear.Regards

  ReplyDelete
 2. hao wari wana mahali pa kuweka hivyo vitu jamani, unaweza kukuta anaenda kupanga chumba kimoja. Makubwa

  ReplyDelete
 3. jaman em tujuze huyo bi salma mntambo anafanya kazi gan mwenzetu had kuturusha roho na hayo madini kiasi hicho. Ikiwezekana fanya nae interview utuwekee hapa ili tujue anajishughulisha na nn na anasave vp pesa zake mpaka anapata na balance ya kununua madini kiasi hicho. Ni muhm ili nac tujpange angalau kumfkia atuwez bac angalau tuwe na tumadini tuwili tutatu loh!!!

  ReplyDelete
 4. Mdau wangu nitafanya naye interview sooon!!!!

  ReplyDelete
 5. naomba kuuliza hv hayo unayosema madini ya mama salma mtambo ni dhahabu zenyewe2 original au zle za kuchovya?

  ReplyDelete
 6. Hizo ni dhahabu za ukweli, na kama wewe ni mtu unaejua kutofautisha dhahabu za kuchovya basi utajua tu...alafu wala aihusu kutaka kujua anafanya kazi gani...wangapi wanavaa dhahabu sijui cha ajabu ni nini.

  Mashallah Mama Salma Mntambo ntakutafuta kwa udi na uvumba nikupe hongera zako na madiini yako ya ukweeee

  ReplyDelete
 7. Nimefurahi kuona Mashughuli blog ipo hewani. Nilipanic pale ilipopunguza makali miezi kadhaa iliyopita, nakutakia mema mamaa, hakuna anayekupita kwa kutuletea habari mkama hizi. Mungu akuzidishie ndugu yangu japo hatufahamiani.

  ReplyDelete
 8. Mashughuli umenikosha sana picha nimezipenda na zawadi zinafurahisha

  ReplyDelete