Katibu wa TA Reading na Mkewe Wameremeta

URBAN PULSE CREATIVE Inawaletea picha za tukio la Harusi ya nguvu iliyofanyika Jumamosi Tarehe 25 septemba  2011 Katika ofisi ya Reading Registrar  kati ya Katibu wa Tawi la TA Hapa Mjini Reading Amri Dello na Alice Kapya.
Baada ya Kufunga pingu za maisha tafrija ilifanyika ndani ya Boat na kuzunguka mitaa ya berkshire hadi  Windsor kwa Queen na kumalizikia katika Mji wa Reading. Wadau mbalimbali walikuwepo katika sherehe hii akiwepo Mh Balozi wetu Peter Kallaghe.
URBAN PULSE inapenda kuwapa hongera sana Maharusi wetu na kuwatakia kila la kheri katika safari yao ndefu walioianza leo.

MUNGU AWABARIKI,

Asanteni

Picha kwa hsiani kubwa ya URBAN PULSE CREATIVE


Boti inayoitwa caversham Princess ikiwasubiri maarusi tayari kwa ajili ya sherehe. 
 Bwana Harusi akiweka Sahihi kwenye cheti cha ndoa
 Bonge la kiss 
 Bwana harusi Dello
 Dello akimlisha keki mkewe
 Kila Kitu kimekwenda poa na jiko nshavuta sasa tugange yajayo

Mh Balozi Kallaghe Akiwa na MH Balozi Kapya wakibadilishana mawili matatu 

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

1 comment:

  1. Ebu sisi tunaopenda kuiga wenzetu. waone maharusi wa majuu, huko ndio kila kitu kipo tena origino hakuna ya kichina kama ipo basi TBS ya kwao imeshapitisha. Sasa neno langu angalia maharusi, nguo simple, make-up natural, jewelery simple, nywele natural. je wamependeza au? sasa sisi huku na joto hili makeup kibao, ma foundation meupe hai yanaonesha mabonde usoni, rangi ndio usiseme tena, na ma shadow yana match na nguo basi pendeza kwenda mbele. Make up hadi ile natural beauty haionekani, tujitahidi zaidi jamani. Mungu ametujaalia tuna ngozi safi nyororo wengine wanaitamani...

    nawapenda...

    ReplyDelete