TANGAZO MAAALUM


JUMUIYA YA WATANZANIA-TANZ-UK ikishirikiana na TA Reading Inapenda kuwakumbushia tena watanzania wote waishio Reading, Slough, Oxford na vitongoji vingine, Kuwa Ziara ya Balozi wetu MH Peter Kallaghe akiambatana na Mama Kallaghe Itaanza rasmi siku ya Ijumaa jioni tarehe 8/4/11 na kuendelea Tarehe 9/4/11 Jumamosi ambapo Mh. Balozi Kallaghe atakutana na Jumuiya mbali mbali za Ki-Tanzania, pamoja na kutembelea miradi na Taasisi mbali mbali za KiTanzania. Wakati Huo huo Mama Kallaghe atajumuika na na akina mama wote Jumamosi kuanzia saa nane Mchana. Kisha Mh Balozi na Mama Balozi watahudhuria hafla kubwa iliyoandaliwa na Wanajumuiya kwa ajili ya kuwakaribisha kuanzia saa kumi na mbili jioni. Bongo DJs watakuwepo wakifanya makamuzi mpaka usiku wa manane. Jumapili 10/4/11 kutakuwa na ibada ya Kiswahili itakayohitimisha Ziara hii ya kipekee. Kutokana na muitiko mkubwa pamoja na ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwa wanajumuia imelazimu kubadilisha ukumbi ili kufanikisha zaidi ziara hii. Anuani ya Ukumbi Rasmi itakuwa WYCLIFFE 233 KINGS ROAD, READING RG1 4LS. Tunawaomba Radhi wote kwa usumbufu uliotokana na mabadiliko hayo muhimu. Tafadhali mjulishe mwenzako na tuzingatie mda. Kwa mawasiliano zaidi kuhusu ziara hii tafadhali wasiliana na wafuatao: Ndg. Hussein 07865673756, Ngd. Upete 07796122127, Mama Maria 07919874182. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu.

mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment