MSAADA WA PILI KUTOKA TIMU YA SAIDIA GONGO LA MBOTO UK WAKABIDHIWA

Picha ya pamoja baada ya makabidhiano
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama (kushoto), akipokea msosi kutoka kwa Doto akiwa Grace Nicolaus.


Timu ya Saidia Gongo la Mboto UK Ikiwakilishwa na DOTO NYADUNDO toka UK ilipeleka msaada wa chakula mapema Jumanne hii ikiwa ni sehemu ya pili ya ahadi zao tatu walizotoa kwa ajili ya kuwasaidia wahangwa wa Gongo La Mboto walishirikiana na bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ walikabidhi msaada wa chakula jumla ya kilo 400 kwa mkuu wa wilaya ya Dar es Salaam Mhe Leonidas Gama. Vilevile Mkurugenzi wa Twanga pepeta iron Lady Asha Baraka alikabidhi michango yao.

Timu ya SAIDIA GONGO LA MBOTO UK imetoa misaada katika makundi matatu:
1. Pesa taslim sh milllion moja na nusu
2. Chakula ambacho kimeshakabidhiwa
3. Nguo, viatu, vitabu na vifaa mbalimbali ambavyo vimepakiwa kwenye kontena tayari kwa safari ya kuja Tanzania
Aidha mkuu wa wilaya ya Dar es Salaam Mhe Leonidas Gama amewashukuru na kuwapongeza watanzania wachache walioko UK waliojitolea kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya kusaidia wahangwa wa Gongo la mboto. Shughuli hiyo ya uandaaji na ukusanyaji wa michango hiyo kutoka Uingereza iliandaliwa na Shilla Frisch, Jestina George kutoka MISSJESTINAGEORGE.BLOGSPOT.COM, Frank Eyembe na Baraka Baraka wa URBAN PULSE CREATIVE na Bernard Chisumo kutoka Locus Impex Shipping Co.mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment