INGIA KATIKA MILANGO MINGI YA KHERI YA RAMADHAAN

Mwezi huu mtukufu umejaa fursa ya kujichumia mengi ya kheri ambayo thawabu zake huanzia tokea kumi hadi zaidi ya mia saba pamoja na malipo maalum yatokayo kwa Allaah kwa Mfungaji, kama alivyosema Mtume

Amesema Mtume Kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake na maji yake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah  kuliko harufu ya misk.

Kwanza kabisa inatupasa tuanze mwezi huu mtukufu kwa kutia Nia moyoni (si kuitamka) yenye Ikhlaasw ambayo ndio msingi wa kutaqabaliwa amali ya ibada yoyote, na ili kupata Ridhaa ya Allaah kama Anavyosema

Ifuatayo ni baadhi ya milango ya kheri ambayo inampasa kila Muislamu ajitahidi kuiingia na kutekeleza hizo amali njema katika mwezi huu mtukufu wenye kheri na baraka nyingi ili kujichumia mema mengi yatakayomfaa mtu Akhera:-

1-Swawm kwa imani Ili Kufutiwa Madhambi:

Amesema Mtume (Atakayefunga Ramadhaan kwa iymaan na kutaraji malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia )) Al Bukhaariy na Muslim.

2-Qiyaamul-Layl (Kusimama Usiku katika Swalah); Tarawiyh na Tahajjud:

Amesema Mtume  (Atakayesimama [kwa Swalah ya usiku] kwa iymaan na kutaraji malipo, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia))

3-Sadaka

amesema Mtume (Sadaqah bora kabisa ni ile inayotolewa katika mwezi wa Ramadhaan)

4-Kumfuturisha aliyefunga:

Amesema Mtume - Atakayemfuturisha aliyefunga, atapata ujira kama ujira wake bila ya kupungua chochote katika ujira wa yule aliyefunga [Ahmad, An-Nasaaiy – Ameipa daraja ya Swahiyh Shaykh Al-Albaaniy]

5-Kusoma Qur-aan sana na kujua maana yake:

Mwezi wa Ramadhaan ni mwezi ulioteremshwa Qur-aan kama Anavyosema Allaah kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi


6-Kukaa kwa kumkumbuka Allaah baada Swalah ya Alfajiri hadi jua litoke:

Imetoka kwa Anas kwamba Mtume (S.W.A) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jama'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhiy na kaisahihisha Al-Albaaniy]


Zaidi ingia AL HIDAAYA

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment