MTOTO MWINGINE WA ADAI MAHITA NI BABA YAKE!

Sophia Mahita (15), mkazi wa Sanya juu, mkoani kilimanjaro, amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la kuingia kwa jinai nyumbani kwa Inspekta Jeneral mstaafu wa jeshi la Polisi, Omar Mahita, akidai ni mtoto wake.
Mshtakiwa huyo alisomewa shitaka hilo jana mbele ya Hakimu Mary Mtoi wa Mahakama ya mwanzo Kinnondoni mkoani Dar es salaam.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa na Karani wa mahakama hiyo, Fatma Khatibu, Machi 23, mwaka huu majira ya saa 3 usiku katika eneo la osterbay, mshtakiwa aliingia kwa jinai nyumbani kwa omar mahita bila idhini yake.
Hata hivyo mshtakiwa aliposomewa shitaka hilo, alikiri kufika nyumbani kwa Mahita, lakini akidai kuwa hakuingia ndani ya nyumba hiyo kama inavyodaiwa bali aliishia nje ya geti.
Mshtakiwa huyo alipohojiwa na hakimu Matoi, aliieleza mahakama kuwa Mahita ni baba yake wa kumzaa na alielezwa hayo na mama yake, Esther Lyatuu, ambaye ni askari mstaafu.
Sophia aliiambia kuwa mahakama kuwa mama yake alimweleza kuwa alimzaa na Mahita pamoja na na ndugu zake wengine wawili wakati wakiwa Sumbawanga mkoani Rukwa.
Sophia aliendelea kuieleza mahakama kuwa aliambiwa na mama yake kuwa walitekelezwa na baba yao (Mahita) wakiwa wadogo, hivyo yeye ameamua kumtafuta baba yake alipo ili angalau aweze kumuona na macho tu na hata ikiwezekana kuongea apate kuongea naye.
Aidha, alieleza kuwa aliambiwa na mama yake kwamba baba yaek ni askari, hivyo alikwenda jijini Dar es salaam kwa kuelekezwa na baada ya kufika kituo cha polisi askari walimpeleka mpaka nyumbani kwa Mahita, lakini walinzi walimwambia kuwa baba yake yuko Morogoro.
"Nilikuja hapa Dar es Salaam nikitokea Moshi kwa maelekezo tu na nilifikia kituo cha polisi ndipo nilipopata msaada toka kwa askari walionipeleka mpaka nyumbani kwa Mahita, baada ya kuwaambia kuwa mimi ni mwanaye." Sophia aliiambia mahakama. Alidai haukupita muda akashangaa askari wamemfuata tena getini na kumkamata na baadaye kumpeleka mpaka kituo cha polisi na kufunguliwa kesi.

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment