Sponsor

MISS TANZANIA - SAGA INAENDELEA!!!! (MIRIAM GERALD)

11:33:00 PM


Pamoja na kusota lupango kwa muda wa siku nne kwa madai ya kufanya fujo na uharibifu wa mali. Miss Tanzania, Miriam Gerald inadaiwa kwa sasa akili yake haijakaa sawa kutokana na kuendelea kuipa nyodo kamati ya miss tanzania. Habari za ndani kutoka kwa mmoja wa wanakamat hiyo, zilidai kuwa mrembo huyo baada ya kuachiwa kwa dhamana, aligoma kwenda kukutana na kamati hiyo ili kuangalia kwa undani tatizo linalomkabili.
Kamati ya miss vodacom tanzania ndio ilikuwa pamoja kuhakikisha mrembo huyo anapewa dhamana, lakini tunashangaa tukimuita hataki kuja kutusikiliza.
Mrembo huyo alikumbwa na kashfa nzito baada ya kubainika kumpora mpenzi wa swahiba yake Miss Tanzania 2008, Nasreem Kassim aitwaye Kennedy Victor.
Nasreem ndio ambaye alimwachia taji la miss mwanza na baadaye la miss tanzania Miriam Gerald na walikuwa marafiki wakubwa lakini baada ya kumpora bwana huyo uhusiano ulikufa kabisa.
Aidha mrembo huyo baada ya kumpata kennedy aliiletea jeuri kamati ya miss tanzania na kumfanya kushindwa kabisa kufanya kazi za kijamii kama ilivyo ada kwa warembo wanaotwaa taji hilo.

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.