MTOTO WA BALOZI AMI MPUNGWE AGARA SOUTH AFRICA!


MTANZANIA, Anisa Mpungwe (24), mkazi wa jijini Dar es Salaam, ameshinda tuzo ya mwanamitindo mpya wa Elle, katika hafla iliyofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Septemba 15, 2009
Shindano hilo liliandaliwa na Kampuni ya Mitindo ya Elle ya Afrika Kusini ambayo hujishughulisha na maonyesho ya mitindo na urembo.
Anisa ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe, kuanzia mwaka 1994 hadi 1999, aliibuka kidedea baada ya kuchaguliwa katika wanamitimndo 100 walioshiriki katika shindano hilo kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, ambapo baada ya mchujo walibaki washindi sita tu.
Kisha washindi hao sita waliweza kuchujwa tena ili kuweza kupata mshindi wa tuzo hiyo ya fahari ya mitindo ya Elle New, ambapo Anisa alitangazwa kuwa mshindi.
Kutokana na ushindi huo, Anisa amejinyakulia kitita cha dola 2000, ambazo ni sawa na zaidi ya sh milioni mbili za Kitanzania.
Zawadi nyingine aliyoipata Anisa katika shindano hilo ni pamoja na kuingia mkataba wa kubuni mitindo kwa ajili ya kampuni ya nguo ya Mr. Price ambapo nguo hizo zinapatikana kwenye nchi mbalimbali linapopatikana duka la kampuni hiyo.
Kwa upande wake Anisa alisema kuwa fedha alizozawadiwa atazielekeza katika kukuza kampuni yake ya uanamitindo aliyoifungua huko Afrika Kusini inayofahamika kwa jina la Loins Clothes & Ashes, ambayo itakua ikibuni mitindo na kuionyesha mavazi katika maonyesho mbalimbali hapa nchini.
Aidha, alisema ushindi huo umetokana na kufanya kazi kwa kujituma na kujiami kwa kipaji chake na kuwashauri wasichana wengine wa Kitanzania kutokatamaa na kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza ndoto zao na kuongeza kuwa kitu kinachotakiwa ni kujiamini kwani ana uhakika ukitilia mkazo katika hivyo utaahinda.
Mashindano ya mitindo ya Elle New huwa yakifanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu ni wa kumi tangu kuanzishwa kwake.
Vigezo vilivyokuwa vikiangaliwa kumpata mshindi ni katika shindano hilo ni pamoja na kubuni nguo kwakutumia wazo la “mapenzi ya kisasa” bila kutumia mambo ya kimapenzi nje nje mfano rangi nyekundu na alama za mioyo.
Anisa ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu wa familia ya Balozi Ami Mpungwe na Anita Rose Mpungwe, alizaliwa Oysterbey, jijini Dar es Salaam mwaka 1984.
Mpaka sasa ana elimu ya stashahada ya Mitindo na Masoko aliyoipata katika Chuo cha Midrand Graduate Institute, pia amehitimu ubunifu wa kunakshi katika chuo cha London College of Fashion.
Uzoefu wake wa kazi ni pamoja na ubunifu wa mavazi ya harusi katika Mellisa Botha, pia amefanya kazi na African Mosaique na katika tukio la Paris Fashion Week.

EBU TUANGALIE AINA TOFAUTI ZA UBUNIFU WAKE
Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment