MSUTO! UKIFANYA HIVI HARUDII TENA!! KUNA HAJA YAKUWAKOMESHA WAMBEA WOTE MIE NIMEIPENDA SANA!

Story hii niliadhiwa na dada yangu anaitwa Afsa, ya kuwa iliwahi kutokea huko Zanzibar zamani saaaana, mtu alikwenda kumkopa shoga yake baada ya kuwa na matatizo amkopeshe pesa kidogo, ninavyosema hivyo shoga yake haswa! wako pamoja kwenye kila jambo liwe la raha au shida, basi yule shoga akampatie mwenzake zile pesa alizokuwa akihitaji, lakini baada ya muda kidogo akaanza kupita mitaani na kuanza kutangaza fulani nimemkopesha pesa zangu, nyumba baada ya nyumba enda akitangaza, muda si mrefu shoga akaipata habari basi bi dada alijitahidi akatafuta zile pesa, akakodi ben na akawaalika wale watu ambao walipewa habari za pesa, saa 7 mchana ben likapigwa na sare juu mpaka kwa shoga na kumlipa pesa zake akamwambia shoga nimefanya hivi kwa sababu ningekupa kimya kimya si rahisi wewe upite kila nyumba na kuwaambia wale wote kuwa nimelipa, na itakuwa kazi ngumu kweli kweli, nimekupinguzia kazi nimewaita ili wajue nimekulipa basi watu wakaserebuka sebene la nguvu.

Sasa basi hii ya leo imetokea Migo Migo au magomeni lakini huyu ni mmbea anasutwa!  embu angalia ucheke haswa na hii pia ni shughuli iko haja ya kuwakomesha wambea maana kuna waambea saaaana ndio mwanamke kuteta lakini isizidi, halafu ukimuona yule ulimteta unajipendekeza kwake mmh! vibaya hivyo

Huyu dada pichani mchana wa leo huko Magomeni kaenda kumsuta shoga yake kisa kamsema tena kwa matarumbeta kafunga mtaa na mpaka wakata viuno kawakodi kwa shughuli hiyo.
Shost hapo anatunzwa pesa na wapambe wake kwa shughuli nzito ya kumsuta yule dada ambae alitonywa na wapambe juu ya kasheshe inayokuja nyumbani kwake hivyo akaingia mitini mapema...
Hapo watu na mzuka wa kusuta.....

Kama kawa utadhani sherehe watu wamepagawa na msuto

Rindima rindima shoga!!!
Mzuka mzuka amenipandisha mzuka!!!!!
shoga alivyopata habari alitoka nduki

Story na picha zaidi mtembelee Dina Marios

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

1 comment: