MWANAMKE NA USAFI

Usafi ni kitu cha msingi sana na chenye kuzingatiwa na kila mtu kwa kila mahali anapoishi au makazi ya watu lakini usafi huu ni ule tunaouona na kuuzungumzia mara kwa mara kama usafi wa mwili na mazingira unayoishi kwa ujumla.Justify Full
Uzuri wa mwanamke si kuwa na shepu nzuri mfano wa muimbaji wa Kimisri, Shakira au J.LO wa Marekani, uwe na nywele laini na ndefu mpaka mgongoni, miguu ya bia, macho kama Ray C au mwenye mapozi ya mwendo kama mwanamitindo wa Marekani, Naomi Campell Lahasha! Bali uzuri wa mwanamke ni ule utakaokufanya uonekane nadhifu na maridadi siku zote au kwa kila mtu utakayempitia mbele yake huku akikusifia kuwa wewe ni mzuri na mavazi yamekupendeza.

Msichana au wanawake wengi wamekuwa wakijiachia sana na kutokujijali bila sababu au wakisubiri kuwe na shughuli kwa rafiki au jirani zao kama vile kwenye harusi, ‘kitchen party’ au ‘send off’ ya shoga yake ndio atafute manukato mazuri ( perfume ), udi, nguo nzuri tena hapo atakuwa ndio ‘kavunja’ sanduku mpaka kuiona nguo atakayokuwa ameipenda na kuona itamfaa au kwenda kwa mama Khadija kuazima mawigi na viatu eti kwa sababu kaalikwa.

Hata hivyo, ukiachana wa wasichana hao, kuna akina dada zetu wenye tabia ya kutokuoga siku nzima au asubuhi wanapokwenda kwenye mihangaiko yao au jioni wanaporudi katika shughuli zao za kila siku na kujidai kuwa wao ndio wao lakini ukimkuta ‘home’ kwake ni kituko, hatamaniki hata kwa bei ya chee.

Vilevile ni busara sana kujiweka katika hali ya usafi kila tunapokuwa karibu na watu hata kama ni ugonjwa basi hauna budi kutafutiwa dawa ili usiendelee kukuumbua.

Huna uwezo hata wa kununua manukato ya kuzuia kunuka kikwapa chako kinachowakera ‘Mashosti’ zako, basi oga angalau mara mbili kwa siku ili kuepuka tatizo linalokukabili na kukutia aibu mbele za watu.

Sio hao tu, hata wale wenye tabia ya kukurupuka asubuhi na kutokupiga mswaki vizuri au kutopiga kabisa eti kwa sababu anawahi foleni ya kwenda kuchukua samaki Feri, huwaachia watu harufu vya mdomo kwenye madaladala na kuwatia kichefuchefu.

Si uungwana haswa kwa sisi akina dada kujiweka katika mazingira hayo ambayo yatakupotezea marafiki kwa sababu kila atakayekuona atakuwa anakukimbia na kutotaka ushoga na wewe, leo naishia hapa, tukutane wiki ijayo.
Ushauri kwa akina dada au mama, mnatakiwa kuwa makini katika mazingira yenu mnayoishi na mwili wako kwa ujumla.

Uzuri na shepu lako halitakusaidi chocho kana utakuwa unanuka na kukimbiwa na wenzako na kukufanya uone kama unanyanyapaliwa kumbe unajinyanyapaa mwenyewe.
Tukutane tena wiki ijayo.

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment