UDI SIFA ZAKE NA MWANAMKE!

kwa wanawake wengi wanaoishi mwambao wa Afrika ya Mashariki manukato ya udi ni sehemu muhimu ya vitu vinavyokuwemo katika vijaluba vya vipodozi vyao. Udi una manukato yanayokaa mwilini na kwenye nguo kwa muda mrefu, na kwa mujibu wa desturi za watu wa mwambao, udi unaaminiwa zaidi kuliko manukato mengine ya kisasa.

Udi ni mchanganyiko wa mti wenye riha, sukari na mafuta ya manukato na huwa ama kama vipande au unga unga. Ukiwekwa kwenye chetezo chenye mkaa uliowashwa na kuanza kufukizwa udi hutoa harufu ya waridi.

Udi unatumika kwa njia mbali mbali na katika matukio mbali mbali. Kutokana na imani za watu wa mwambao, vyumba vilivyofukizwa moshi wa udi haviwi tu na harufu ya waridi bali pia hukaribisha ruhani wazuri nyumbani.

engi wa wanawake wa mwambao hutumia udi katika makabati yao ya nguo na katika masanduku kama njia ya kuzipa manukato nguo zao.

Udi pia unatumiwa zaidi kama chambo au kivutio cha mapenzi kwa wanaume wa pwani ni aina ya kishawishi cha kuamsha ‘ashki’ ya wanaume.

Kwa kawaida kila jioni baada ya kuoga wanawake wa mwambao hujifukiza udi bila kujikausha maji katika miili yao.

Udi hufukizwa kwa kuchutama au kusimama ukiwa umepanua miguu na katikati yake kuwekwa chetezo chenye mkaa unaowaka na udi kufuka moshi, ni lazima kutumia ‘khanga’ ‘kitenge’ na hata ‘shuka’ kufunika mwili ili kuzuia moshi wa udi usitoke.

Ingawa kumekuwa na maendeleo ya teknolojia ya utengenezaji wa vyetezo vya umeme na ambavyo ni rahisi kwa kujifukiza, wanawake wengi wanapenda kutumia njia ya asili ya kujifukiza udi kwa kutumia mkaa

Udi hutumika sana wakati wa ndoa na sherehe nyingine za kidini. Ni kitu cha kawaida kwa bibi arusi na bwana arusi kutumia udi.

Kwa kawaida vazi la bibi arusi na nguo zake nyingine anazokwenda nazo kwa mumewe hufukiziwa udi.

Wanawake wengi hujifukiza zaidi udi wanapokuwa katika siku za mwezi ili kuondoa harufu mbaya ya damu ya mwezi.

Na ni sifa kubwa kwa mwanamke hukajifukiza udi ukolee na ukipita pahali basi ukaacha harufu ya udi hata kama hutoambiwa basi lazima hutapata sifa sana, mwanamke yule ananukia udi
Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments:

Post a Comment