Sponsor

,

NAOMI ALIPOTEMBELEA WARD YA WAZAZI M-NYAMALA

12:07:00 AM

Super Modal Naomi alitembelea ward ya wazazi pale hospital ya mwananyamala, alishindwa kujizuia chozi baada ya kuona jinsi wamama wajawazito walivyokuwa wakijifungua kwenye hali ngumu hali inayoweza kusababisha kupoteza maisha ya mama na mtoto.
Aliona wamama wakiwa wamelundikana kwenye sakafu na vichanga vyao mikononi na wengine wakiwa wamelala hata watatu na vitoto vyao kwenye kitanda kimoja.
Naomi alitoka nje ya hospitali na kwenda chini ya mti na kuanza kulia kwa uchungu huku wapambe wake wakimbembeleza, hiyo ndio hali halisi ya maisha ya bongo tena sometimes unaumwa na uchungu hakuna nurse ya kukusaidia kujifungua kuna cases nyingi tu kina mama wajazito wamepoteza maisha yao na vichanga vyao baada ya kukosa huduma muhimu pale tu anapoanza kuumwa na uchungu, na matukio kama haya hapa Dar yanotokea katika hospital kubwa tu, usishangae ndio tunavyoishi wabongo, je maisha bora kwa kila mtanzania tutafikia kweli au bora maisha kwa mtanzania

You Might Also Like

0 comments

SUBSCRIBE NEWSLETTER

Get an email of every new post! We'll never share your address.