BAIBUI LA UKAYA

Hii ni aina ya baibui ambalo mabibi zetu walikuwa wakivaa zamani sana kuweza kutoka kwenda sehemu zote, nikamaanisha kwenye arusi,mazikoni, sokoni na kwa wakati hii wa sasa ni nadra sana kukutana na mtu amelivaa si mabibi hata hao wasichana watu wamezoea mabaibui ya kawaida, lakini juzi alinikumbusha mbali sana Designer Bahiya Lumelenzi kwani alilitoa lili baibui la ukaya na akalibadilsha katika kitambaa cha kawaida, ikumbukwe hapo zamani yalikuwa ni katika kitambaa cheusi tu, lakini kwa sasa waweza lishona katika rangi yoyote upendayo na ukavaa na nguo na likapendeza sana!, inabidi tuwe na siku ambayo itaitwa Swahili fans day, watu wote tunakwenda tumevaa nguo zetu za kiafrika za zamani ili tuweze kukumbushana mavazi yetu ambayo yanatokomea kabisa katika karne hii, hakika kuna uwezo mkubwa wa vizazi vyetu kutokujua kuhusu mavazi ya yetu ya zamani mfano mnzuri ni hili baibui la ukaya, basi ukimkuta mwanamke wa pwani amevaa baibui lake anakwenda sokoni hakika utampenda na nzuri kwa sababu lina sitiri mwil wa mwanamke vinzuri,

Mashughuli

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

1 comment:

  1. It is true our heritageE ARE going to perish and disappear when we will not take consideration to promote them, So I warmly welcoming you to work with me to keep these heritage dresses as a part and parcel of our tangible and intangible African Heritages alive.

    NB please I ENCOURAGE YOU TO USE SINGLE LANGUAGE whether Kiswahili or English in your next Publishes avoid KISWA-GLISH


    for more information please visit Litimbafashion.blogspot.com or 0714388543

    ReplyDelete